Jumatano, 15 Mei 2024

PRETTY SONG OF MY SOUL


 

Bora kuumaliza muda wangu nikitumaini,

Nikitumaini yafanyike Duniani kama mbinguni,
Mbinguni kama Duniani katika mji mpya.

Nafsi yangu imechoka kushindana na Mungu,
Kama alivyosema hatoshindana tena nami,
Kwa kuwa nimeruhusu kuwa mpumbavu.

Nimedondoka katika utukufu kwa kujitakia,
Sikumbuki nilipotoka na namna ilivyokua,
Ila kuzaliwa kwangu ilikua ni vita.

Waliniita Kashinde kwa kuwa hawakutarajia,
Walipoteza tumaini nilipowapa matumaini,
Nimezaliwa natembea sijadondoka.

Natamani sasa kuelewa kwanini nipo hapa,
Kwanini ilikua vita hata sasa bado ni vita?
Je? Nitaondoka nikiwa nimelala au ntatoweka.

Ni kweli sikiamini kifo kwa kuwa ni usingizi,
Nachoogopa ni huu mwili kuoza hainivutii,
Sipaswi kuipenda nguo hii kuliko mwili wangu.

Bado sikiamini kifo kwa kuwa ni usingizi,
Nachukia napolala nikiwa sijui kama nimelala,
Kwanini nipitiwe bila kumjua anayenipitia?

Mlalo ni mapumziko kifo ni sawa na likizo,
Mtu anayeishi ajawahi kutulia na kupumzika,
Akipumzika amekufa Je? Kifo ni Nini?

Kama ni hivyo kifo ni uzima na uzima ni kifo,
Wapumbavu tunakosa jicho la kutambua,
Kwamba atakalo lifanyike hapa kama kule.

Usijisumbue aliye juu mngoje chini sana,
Na aliye juu akungoje chini nyote ni sawa,
Paradiso ni katikati ya kuharibika na kutoharibika.

Photo Credit @thecyclopssun

Alhamisi, 9 Mei 2024

INANI NI CHAGUO ILA CHAGUO SIO IMANI

 


Imani ni machaguo, Unakua unachokiamini kwa kuwa kila unachokiamini ni ukweli na sio ukweli.

Sisi sio waumbaji ila ni waumbaji kwa kuwa yupo muumbaji aliyeumba na kutupa nguvu ya uumbaji.

Ndiyo au Siyo yote ni majibu sahihi katika kila kitu, Tunaishi katika ulimwengu usio na mipaka.

Wanaothibiti mwili wamejiwekea mipaka kwa kuwa wao sio kama sisi wao ni kwa njia ya mwili.

Huu mwili sio kitu bila hisia ndio maana wanacheza na hisia zetu kwa kuwa hisia hutibua mambo.

Muombe Mkuu aliye sirini akupe nguvu ya kumshinda hisia, hofu na upofu kwa kuwa hawa ndio adui zetu.

Mpaka sasa ninapoandika ujumbe huu nipo katika vita kwa kuwa vita vyetu sio katika damu na nyama bali roho.

Vita vyetu ni dhidi ya Ujinga na Utumwa wa Mwili, Vita vya Mtu wa ndani na Mtu wa Nj'e ambaye sio ukweli ila ni Ukweli.

#GeneTZA #Gnosis #Seekers #2024

Jumamosi, 20 Aprili 2024

WATAWALA AKILI WAMEUPATA MWILI



Watawala Akili Wameupata Mwili.

Maadui wakubwa wa hii Dunia,
Ni Shule, Dini, Wanasiasa na Utamaduni,
Utamaduni ilikua zamani sasa ni mitindo,
Shule zilikua familia sasa ni madanguro,
Dini zamani ilikua imani sasa ni biashara.
Siasa ni programu ya kishetani sio maisha,
Nchi ina majeshi saba bado watu wanaibiwa,
Majeshi yao ni kwaajili yao kutulinda watumwa
Government (Govern - Mental) Tafakari Sana,
I'AM self govern man I'AM kila Mtu sote pia.
Serikali ni kila mmoja wetu sio wachache,
Walioshika mpini tuliowapa kutuadhibu sisi,
Wao ni Conscious sisi ni Unconscious kiini,
Bila sisi hakuna wao wachache wanajua hili,
Hivyo wamepanga kuturubuni na kututenga.

Jumatano, 17 Aprili 2024

MAFUMBO KATIKA MAUMBO YA ULIMWENGU

 


Mfalme Sulemani Naye Ni Metaphor (Fumbo).

Mwezi unawakilisha siku,
Jua linawakilisha majira,
Nyota zinawakilisha miezi,
Miili yetu ni hekalu la Mungu,
Solar/Soul - Moon/Mind = (Solomon).
Maneno yanawakilisha herufi,
Herufi zinawakilisha sarufi na mafumbo,
Ndio maana zikaitwa Alphabet (Alpha-Better),
Lugha waliyopewa vinega ktk ngome (caves)
Kwa kuwa hawawezi kuwasiliana kiungu.
Kuwasiliana kiungu ni kutumia telepathy,
Wengi wanaijua hii, Unaweza kusoma kitu,
Kusoma bila kufungua mdomo (telepathy),
Kuna baadhi ya binadamu hawawezi hii jaribu,
Zungumza bila kufungua mdomo kimawazo.

Kila kitu ni umeme na nguvu ya uvutano,
Umeme ni mme, Mvuto ni mke (Electromag.),
Mungu ukoo wake ni Elohim (EL) Electricity,
Katika tafsiri tunasema EL O HIM (Elohim),
Ibrahim alimuabudu Mungu huyu (Miungu).
Aliye juu ni mmoja baba yetu An (Anu),
Unaweza kumuita The Most High God,
Jina lake la siri A'lyun A'lyun EL The Most High
Wengine wanamuita Allah, Eloh, Elyon, EL.
Vipi kuhusu Sabaoth,Abraxas na Yieldabaoth?
Hawa viumbe wanaishi miaka mingi,
Hawana jina moja kama Yesu, Nimrod, Apollo.
Yesu naye ni wa ukoo wa Elohim (Emmanuel)
Emm-anu-el (Yeye na Baba ni Wamoja)
Nadhani hapo unanipata vyema Break Spells.

Binadamu tuna mifumo tano ya fahamu,
Vidole vitano n.k Namba ya mabadiliko,
1234 (5) 6789 Kundi la kwanza ni mbingu,
Kundi la pili ni kuzimu (matter/material),
Inatakiwa u-balance mema na mabaya.
Ukisikia Mungu ni katikati ya uzima na kifo,
Ndio hapo sasa!!!

Jumamosi, 13 Aprili 2024

IT WILL NEVER STOP TILL WE BACK ON OUR SEAT.



Hata sasa tunajua kuwa hakuna Middle East,
Hakuna Israel wala Palestina, Yote ni Afrika,
Shetani alitugawanya na kuweka mipaka,
Akachimba mfereji wa Suez Canal kututenga,
Na bado ameendelea kuitenga kaskazini yetu,
Ameifanya ya waarabu na kutawanya wanya.
Hao miungu wa Kigiriki wasio tahiriwa,
Walitufanya tuziache njia zetu za kale,
Tumemkataa Mungu kwa tamaa ya najisi,
Baada ya Malaki kabla ya Matayo wakaficha,
Wakauficha ukweli, Miaka 400 ya ukimnya,
Ukatolewa ukweli wa Maccabees katika biblia.
Deuteral Canonicals (Walipozika Ukweli),
Historia ya yaliyojiri katika damu na nyama,
Ndugu zetu walivyomsaliti Mungu na kujitenga
Wakaoa wake wa kigiriki na kutotahiriwa hata,
Ole wako wewe uliyeoa adui akakufanya,
Akakufanya umuache Mungu wa Babu zako.
Unyama wa Alexander wa Macedonia,
Na vijana wake waovu waivyotawala Dunia,
195 B.C.E (Greek Invasion In Africa),
Wagiriki walipoivamia Israeli (Afrika) zamani,
North East Africa (6 Century A.D) Hakukua,
Hapakua na wayahudi bado kumbuka (Africa),
Kama kawaida baadhi wakauza utu wao kwao
Wakaacha njia zao za asili na kutotahiriwa,
Ili kuonekana kama hao sio sisi bali njia yao,
Multi Culturalism watu wote kuwa wamoja,
Ila ni uongo tuliacha yetu tukafuata yao,
Hata sasa sisi sote tumezaliwa katika Uongo.
Hellenization (Hell On Earth) Hapa ndipo,
Ndipo tulipo waacha manabii zetu,
Tukaruhusu manabii wao kuwa manabii zetu,
Na manabii zetu kutokua manabii zetu tena,
Fuatilia historia ya Greco-Roman Government
Nimepaa juu ya walinzi wa mageti ya kuzimu.
Nitaushuhudia ukweli uliofichwa katika Giza,
Hao wanaojiita Israeli wanajua kuwa wao sio,
Sio waliomkataa Kristo bali watu weusi sisi,
Tulipokea Yesu Mzungu na Kumuacha Mungu,
Imeandikwa siku ya mwisho mtamgongea,
Mkisema bwana bwana mbona tulitoa pepo.
Tulitoa pepo kwa jina lako atawaambia sikujui,
Ushaidi sio huo tu nenda kasome kuhusu,
NEANDERTHAL (Ukweli Utakuweka Huru),
Lovers Of Sophia (Mruhusu Roho Akuongoze)
Mpende Roho Mtakatifu nae atakuongoza,
Huyo pekee ndio Mwalimu wa kweli.

DAYS/WEAK (WEEK)


Monday - Moon
Sunday - Sun/Sol
Tuesday - Mars/Tui
Wednesday - Woden/Mercury
Thursday - Jupiter/Thor
Friday - Frygga/Wife Of Odin (Venus)
Saturday - Saturn/Satan (Kronos)
Alafu Unaniambia Unaabudu Mungu Mmoja Hahahah 😂😂😂 Hii Dunia Hai-Make Sense Kabisa, Everything Is Lie.
We Are Worshiping Star's ✨ (Babylon) Kwanini Watufiche??? Waislamu Mwezi Unaandama 🌙 Wakristo Wapo Na Sun/Son Of God🌞

KQE PODCAST WORD 0011/ IMANI NI MACHAGUO (FREE WILL)



Kashinde Quotes Explanation Podcast (KQE Podcast Word 0011) - Imani Ni Machaguo (Free Will).

Wakuu wa hii Dunia wametuaminisha vingi,
Wametufanya tuamini katika majira na saa,
NDIO maana MIILI yetu INAKUFA tumejitakia,
Imeandikwa kwenye Biblia msifuate majira,
Wapumbavu binadamu kwani tunasikia.
Wakuu wa hii Dunia wametufanya tuamini,
Tuamini kuwa mwaka mmoja una siku 365,
Wakati kihualisia ni siku saba (7) tu zinajirudia,
Unaishi siku saba ukiamini kuwa ni MWAKA,
Ujiulizi kwanini watu wanakufa mapema now.
Wakuu wa hii Dunia wametuaminisha vingi,
Wametuaminisha kuwa siku zipo saba tu,
Nane na tisa wakazifukia kwa matumizi yao,
Wametudanganya Chakra zipo saba pia,
Elements za binadamu ni tano hakuna Ether.
Wakuu wa hii Dunia wametufanya tuamini,
Tuamini kuwa tunapaswa kula x3 kwa siku,
Eti tusipokula tutakufa lakini hawatuambii,
Kitakachotuua ni Addition ya chakula (uraibu),
Asilimia 99 Ya Binadamu Ni Waraibu Wa Diko.
Wakuu wa hii Dunia wametuaminisha vingi,
Wametuaminisha kuwa Bangi ni mbaya,
Sigara na Pombe za majini (Gin) ndio nzuri,
Sio kama naisifia Bangi usivute kama una akili,
Kila mtu ana akili ila tatizo ni Discipline.
Wakuu wa hii Dunia wametufanya tuamini,
Tuamini kuwa Mwanamke ni kiumbe dhaifu,
Mwanaume ndio shupavu wa nguvu za mwili,
Ujui mke M-1 anaweza kuridhisha waume 10,
Je! mume mmoja aweza kuridhisha wake 10?.
Wakuu wa hii Dunia wametuaminisha vingi,
Wametuaminisha kuwa Mungu sio mweusi,
Wametufundisha kukemea nguvu za Giza,
Bila kujua kuwa tunajikemea sisi wenyewe,
Hakuna MWANGA bila GIZA, kuna Giza bila...
Wakuu wa hii Dunia wametufanya tuamini,
Tuamini kuwa Dunia ni Globe/ Tufe/ Duara,
Wakati Dunia ni Sahani/ Chapati/ Duara,
Wametuaminisha Dunia inazunguka Jua,
Wakati kila siku tunaona jua linazunguka hapa.
Wakuu, Wakuu Acha Niishie Hapa.
Wametuaminisha ukipenda mke ni mmoja tu,
The One And Only, Mungu sio Only ila ni One.
One In A Million, Billion, Trillion....
Wanatufundisha Ubinafsi Ni Mapenzi Hah!!!

PRETTY SONG OF MY SOUL

  Bora kuumaliza muda wangu nikitumaini, Nikitumaini yafanyike Duniani kama mbinguni, Mbinguni kama Duniani katika mji mpya. Nafsi yangu ime...