Jumapili, 8 Desemba 2024

Genesis 1 - Shadow & Snakes.

 

Cembe 2401


Nimeufanya mwanga kwa kinywa changu,

Na kunuwia utukufu ndani ya roho yangu,

Nimelichora Ua Kwa nafsi yangu, 

Na kulikabili Giza kwa Moyo wangu,

Nimevishinda vita vya kichwa changu,

Kwa kujitoa sadaka mwili wangu.


Nimeziumba picha kwa macho yangu,

Na kuzichambua taswira kwa fahamu zangu,

Nimeishi katika mbingu kwa haki yangu,

Na kuonja matunda ya utukufu kwa midomo yangu,

Nimeumeza uzima kwa kinywa changu,

Na kushiba umilele katika nafsi yangu.


Kila nilichokitaka nimekipata,

Kila nilichokipata nilikitamani,

Kila nilichokitamani nimekijua,

Kila nilichokijua hakikua kama nilivyojua,

Kila nilipojua nilijifunza, 

Kila nilipojifunza sikujua,

Kila nisipojua sikutambua, 

Kila nilipotambua nilikosea.

Kila nilipokosea nililia, 

Kila nilipolia nilicheka,

Kila nilipocheka nilizimia, 

Kila nilipozimia nilikufa,

Kila nilipokufa niliishi, 

Kila nilipoishi niligeuka Mnara wa Chumvi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Genesis 1 - Shadow & Snakes.

  Cembe 2401 Nimeufanya mwanga kwa kinywa changu, Na kunuwia utukufu ndani ya roho yangu, Nimelichora Ua Kwa nafsi yangu,  Na kulikabili Giz...